Watu wenye Albinism wakiwa katika Mkutano
Mhadhiri wa sheria wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Dkt. Abdallah Posi ameshauri kuwepo kwa ushirikishwaji wa watu wenye albinism katika masuala ya ubadilishaji au utungwaji sheria ambazo zitasaidia kuwalinda.
Dkt. Posi amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa watu wenye albinism kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika, wenye lengo la kuangalia changamoto za watu wa jamii hiyo na ni jinsi gani zinaweza kufanyiwa kazi na serikali za nchi wanazoishi.
Amesema katika ushirikishwaji wa makundi hayo kwenye masuala ya kisheria ni lazima wawepo wataalam ambao wataweza kuwasaidia kuwaeleza vifungu kadhaa vya sheria kwa lengo la kuwapa uelewa zaidi.






