
Mkuu wa polisi nchini Tanzania, IGP Ernest Mangu.
Wakizungumza na wafanyakazi Mwenyekiti wa kanda wa chama cha Wafanyakazi wa Reli nchini (TRAWU) Bw. Yusuph Mandai na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya wanawake (TUCTA) Bi. Rose Mwambe wamesema kuwa hawapo katika mgomo ila wanashinikiza uongozi kuwasikiliza na kuwalipa mshahara, na kudai kuwa
mpaka Serikali itakapowalipa mishahara yao ya Februari hadi Mei ndipo watakapoendelea na kazi.
Naye mmoja wa wafanyakazi hao ameeleza kuwa wao ni watoa huduma kama wengine na hawawezi kufanya kazi kama hamna chakula na kuongeza kuwa kutolipwa kwao mshahara kumewaathiri kiuchumi.
Mgomo huo umesababisha kuahirishwa kwa safari za Dar es Salaam kwenda Kapirimposhi Zambia na Dar es Salaam na Mwakanga mpaka madai yao yatakaposikilizwa.
Wakizungumza na East Africa Radio abiria Joyce Godfrey na Hasani Mwera wamesema walitegemea kusafiri kesho lakini wamefika hapo na kuelezwa kuwa huduma ya usafiri imesitishwa kutokana na mgomo wa wafanyakazi.