Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi ,Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao wamekuwa wakifanya matukio ya ujambazi kwa muda mrefu na kupelekea jeshi hilo kuwasaka bila mafanikio hadi walipowakamata.
Kamanda Mutafugwa ameeza kwamba watu hao wamekamwatwa na bunduki aina ya shortgani pamoja na mapanga na vifaa ambavyo vinaweza kuvunja kufuli la aina yoyote.
Aidha majambazi hao baada ya kutakiwa kutoa taarifa za wanakohifadhi silaha zao wamemtaja mkazi mmoja wa Majengo Mjini Moshi ambaye ni raia wa kihindi ambaye ndiye huwahifandia silaha kwa muda mrefu.
Aidha Kamanda Mutafugwa amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kutoa taarifa za uhalifu zinazotokea maeneo yao pamoja na watu watakao wahisi kuwa na dalili za kutokuwa watu salama katika maeneo yao ili jeshi hilo liweze kufanya kazi yake.