Wednesday , 30th Jul , 2014

Jumla ya maboksi 568 yamekamatwa na jeshi la polisi Kagera yakiwa na vipodozi haramu pamoja na dawa za binadamu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Henri Mwaibambya

Jumla ya maboksi 568 yamekamatwa na jeshi la polisi Kagera yakiwa na vipodozi haramu pamoja na dawa za binadamu.

Akiongea mkoani Kagera kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa huo Henri Mwaibambya amesema vipodozi hivyo vimekamatwa  katika tarafa ya Bugabo wilayani Bukoba vikiwa ndani ya ziwa Victoria vikiwa vimeingizwa nchini kutoka nchi jirani ya  Uganda kwa njia ya magendo huku vikiwa vimepakiwa ndani ya mtumbwi wa mbao wenye namba za usajili TMZ 010078.

Kamanda huyo amewataja watuhumiwa walio kamatwa kuwa ni Otanga Jaluo- miaka 34 mkazi wa Pasiansi Mwanza, Yusuph Juma- miaka 46 mkazi wa Mwanza na Eleven Sylivester Msimbiti - miaka 43 mkazi wa Mwanza pia.
 
Aidha kamanda huyo wa jeshi la polisi amethibisha kutokea kwa kifo cha mauaji ya mtoto mchanga mwenye umri wa miezi tisa aitwae Angel Abeid, ambaye ameuawa usiku wa kuamkia leo  na mama yake mzazi Vaileth Kalumuna (miaka18).

Ameongeza kuwa mama huyo alimbana pua na mdomo mtoto huyo hadi akapoteza maisha, na baada ya kuhojiwa na jeshi la polisi mama huyo alieleza chanzo cha kumuua mwanaye kuwa ni ugumu wa maisha