Wednesday , 25th Feb , 2015

Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ameahidi kuchangia sh. milioni 295 ili kufanikisha ujenzi wa miundombinu katika mradi wa umwagiliaji uliopo kwenye Kijiji cha Nundwe, Kata ya Ihalimba, Wilaya ya Mufindi, mkoani iringa.

Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda.

Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ametoa ahadi hiyo baada ya kupokea taarifa ya mradi, kuukagua na kuelezwa changamoto zake.

Amesema mradi huo ukikamilika utaleta tija kwa wakulima ambao wataongeza uzalishaji wa mazao hasa kwenye kilimo cha malimbichi kama nyanya, vitunguu, viazi mviringo na kukuza kipato chao.

Akielezea manufaa ya mradi huo, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Bw. Mahmood Mgimwa, amesema utakapokamilika utanufaisha kaya 666 zenye zaidi ya wakazi 2,000 katika kijiji hicho na kaya 3,000 zenye wakazi 13,000 kutoka vijiji vya Kata ya Ihalimba na Ifwagi.

Ameongeza kuwa, mradi huo umeanzishwa na wananchi kutokana na miundombinu duni ya umwagiliaji kwa kutumia njia za asili ambazo tija yake ni ndogo kwenye udhibiti wa maji.