Thursday , 7th Apr , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Ntibenda, amewataka wanaomiliki silaha za moto bila kuwa na vibali kuzisalimisha silaha hizo katika vituo vya polisi ili kuepuka matumizi mabaya ya silaha yanayoweza kuchochea vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda.

Arusha ni mkoa unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaomiliki silaha kutokana na uwepo wa Wafanyabiasha wakubwa wakiwemo wafanyabiashara wa madini ya vito aina ya Tanzanite.

Ntibenda ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wenyeviti wa mitaa na Watendaji wa serikali za mitaa katika wilaya ya Arusha mjini ambapo amesema kuwa kwa sasa amesitisha kusaini vibali vya kumili silaha mpaka pale zoezi la uhakiki wa silaha na usalimishwaj.

Mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku uuzwaji wa pombe aina ya viroba na kuwataka viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana vyema na viongozi halmashauri katika kusimamia maagizo ya serikali ili kusukuma gurudumu la maendeleo.

Kwa upande wao Wenyeviti wa Mitaa Jacob Meja Mwenyekiti wa mtaa wa Baraa na Sara Mrema Mwenyekiti wa Majengo A wameiomba serikali iwaboreshee mazingira ya kazi kwani wamekua wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutolipwa posho na kutokua na ofisi.