Monday , 7th Jul , 2014

Watanzania wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wa kushuka kwa thamani ya shilingi kutokana na kubadilishwa kwa noti ya shilingi 500 kuwa sarafu kwa kuwa thamani yake itabaki pale pale.

Noti ya Shilingi mia tano

Watanzania wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wa kushuka kwa thamani ya shilingi kutokana na kubadilishwa kwa noti ya shilingi 500 kuwa sarafu kwa kuwa thamani yake itabaki pale pale.

Akizungumza na East afrika Redio leo Mhadhiri wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam na mchambuzi wa mambo ya siasa na uchumi Dk. Benson Banna, amesema kuwa kushuka kwa thamani ya shilingi kunategemea zaidi kutetereka kwa thamani ya dola ya Marekani ambayo nchini nyingi zinaitumia.

Banna amesema kupotea kwa sarafu kunatokana na kushuka kwa thamani ya shilingi na sio kubadilisha noti kwenda sarafu na kubainisha kuwa sarafu zote zilizopotea ni kutokana na kushuka kwa thamani katika manunuzi.