Wednesday , 24th Feb , 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa akiwa ziarani nchini Burundi amekutana kwa mazungumzo na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ambapo Ban amesema rais huyo ameahidi kuondoa vikwazo dhidi ya vyombo vya habari, na kuwaachia huru wafungwa 1,200,

Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon wakiongea na Waandishi Mjini Bujumbura.

Kwenye taarifa yao kwa vyombo vya habari Rais Burundi, Pierre Nkurunziza amekiri mchango mkubwa wa Umoja wa mataifa katika juhudi zake za kustaawisha taifa hilo, na kuwa amekubaliana na mgeni wake Ban Ki Moon kuondoa changamoto njiani na kuhakikisha amani na usalama vinatawala nchini na kuanzisha mazungumzo jumuishi na wadau wote wa kisiasa katika kuutanzua mgogoro wa kisiasa nchini humo.

"Wametuomba tuzidishe juhudi katika kuimarisha haki za binaadamu, kuhusu pia kupambana na ugaidi na kupiga vita umasikini pamoja na mipango mingine ambayo tunashirikiana na wafadhili ikiwa ni pamoja na mashirika ya Umoja wa mataifa . Hii itatudadia katika ujenzi wa taifa la amani na usalama"

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemchagiza Rais wa Burundi na serikali yake kuanzisha mara moja mazungumzo jumuishi na pande zote.

Ujumbe huo ndio pia Ban ameuwasilisha akikutana na viongozi wa kisiasa na kujenga imani kubwa.

CHANZO BBC