Friday , 13th Nov , 2015

Mkoa wa Njombe umejipanga kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa kusambaza vipeperushi vya kujikinga na ugonjwa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi

Akizungumza na kituo hiki, afisa wa afya mkoa wa Njombe, Mathias Gambishi amesema kuwa katika mkoa huo ugonjwa huo bado haujaingia kutokana na mkoa huo kufanya vizuri katika usafi wa mazingira.

Amesema kuwa katika mkoa huo hakujapatikana mgonjwa hata mmoja wala mtu mwenye viashiria vya ugonjwa huo na kuwa wananchi asilimia kubwa wamepatiwa elimu kupitia wataalamu wa halmashauri za mkoa huo.

Ugonjwa wa kipindupindu ulianza jijini Dar es salaam na kusambaa katika baadhi ya maeneo ya mikoa mingine 18 hapa nchini na kuua watanzania na wengine kulazwa.