
Moja kati ya mgonjwa akifanyiwa vipimo.
Upimani huo umeandaliwa na Hospitali ya Muhimbili, tawi la Mloganzila, kwa kushirikiana na Chama cha Wataalamu wa Matumizi ya Mionzi katika Uchunguzi na Tiba Tanzania (TARA) ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Wataalamu wa Mionzi Tiba Duniani.
Mtaalam wa Radiolojia, Dk. Lulu Sakafu, amesema kadri umri unavyozidi kwenda juu, wanaume wanakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, hivyo wanashauriwa kujenga utamaduni kwa kupima afya zao mara kwa mara.
Amesema watu wasiofanya mazoezi wako katika hatari ya kupata matatizo tezi dume na kwamba wanaume wanaopenda kula chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta pia wako katika hatari hiyo. Alisema wengine wanaweza kupata ugonjwa huo kutokana na historia ya familia zao.
"Katika madhimisho ya mwaka huu, tumeamua kupima tezi dume kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 ili kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa huu kwa sababu kansa ya tezi dume duniani inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo kwa wanaume,” amesema Dk. Sakafu.
Akizungumzia dalili za tezi dume, Dk. Sakafu alizitaja kuwa ni pamoja na kupata shida wakati wa haja ndogo, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza haja ndogo, kujisaidia mkojo wenye mtiririko