
Rais Magufuli (katikati usawa wa kamera) akisalimiana na baadhi ya wageni waliokuwa katika hafla hiyo.
Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo akiwa jijini Mwanza kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Meli mpya na Chelezo katika Ziwa Victoria, ambapo ujenzi huo utagharimu shilingi Bilioni 88. 76.
''Mimi nitawapa hizo bilioni 3.7 ndani ya wiki mbili, sasa ole wenu msifanyekazi tena mtazitapika, nawaambia kabisa huu sio muda wa kubembelezana lazima tubanane kwa sababu tumechelewa'', ameonya Rais Magufuli.
Wafanyakazi hao wanadai malimbikizo ya mishahara ya takribani miezi 27 ambapo Rais Magufuli ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa uendeshaji wa sasa wa Marine Service chini ya Kaimu Mkurugenzi Erick Hamis.
Rais yupo ziarani katika mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Mara ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.