Mama Mghwira ameyasema hayo alipokuwa akishiriki katika kipindi cha 'Wanawake Live' kinachorushwa na EATV. Mwana mama huyo ambaye aligombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi October 2015.
Kuhusu kumuunga mkono Rais Dkt.John Magufuli Mghwira amesema chama chake kitazidi kumuunga mkono na kushikamana naye katika mambo mazuri atakayotekeleza kwa manufaa ya watanzania pamoja na kukumbushia ahadi ambazo Rais aliziahidi wakati wa kampeni ili aweze kuzitekeleza kwa vitendo.
''Rais asipopata watu wa kumkumbusha mara kwa mara kuhusu ahadi alizo ahidi anawerza sahau baadhi ya vitu muhimu, na wanasiasa kila mmoja huwa ana matamanio yake binafsi hivyo lazima tutimize wajibu wetu''Amesema mama Mghwira.
Aidha Mghwira amesema kwa sasa amejikita katika mambo kadhaa ikiwemo kusaidia wanawake kuwa viongozi na kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.





