
Mlinga ameyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo aliomba muongozo kwa kiongozi wa shughuli za Bunge Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kuhusiana na jambo ambalo limetokea ndani ya ukumbi wa Bunge.
Naibu Spika akatoa nafasi kwa Mbunge huyo kuweza kuomba muongozo aliotaka ambapo amesema kwamba leo asubuhi wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje Mbunge Anatropia akiongozana na wabunge wengine wa Chadema walifika katika meza yake na kumvua kofia yake na kutokomea kusikojulikana.
Kitendo hiki kimenisababishia mtikisiko wa mawazo kwa sababu sikujua alikuwa na maana gani na kwa muda amewakosea wananchi wa jimbo langu,
Amelikosea heshima vazi hili kwa kuwa anayetakiwa akuvue kofia hii ni mke wako wa ndoa hivyo amemkosea mke wangu mama Glory kwa kumuingilia katika himaya yake, na hata hivyo amevunja msimamo wa wabunge wenzake kwa kunijongelea.
Ametoa maelezo marefu kuhusu jambo lake na akauliza kama vitendo hiki kinaruhusiwa na kwa kuwa alimvua akiwa bungeni ina maana angekosa sifa ya kuwa bungeni kwa sabbabu kanuni zinataka Mbunge akivaa kanzu avae na baraghashia.
Naibu Spika ameongeza kuwa kwa kuwa jambo hilo hakuliona anakwenda kulifanyia kazi na atajibu mwongozo huo kwa kuzingatia hoja alilozitaja.