Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti ya Uchaguzi kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adam Nyando, amesema kuwa maandalizi ya mchakato huo yanaanza kwa kufanyia maboresho makubwa sheria ya kura ya maoni.
Afisa huyo amesema kuwa kikubwa kwa sasa kinachofanywa na tume hiyo ni kuendelea kutoa elimu kwa mpiga kura ili kumpa ufahamu mwananchi juu ya kutambua haki yake ya kupiga kura.
Tume hiyo ya Taifa inaendelea na zoezi hilo la kukabidhi ripoti ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu iliomalizika Octoba 25 mwaka jana kwa mikoa mbalimbali hapa nchini na jana ilikabidhi katika mkoa wa Pwani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiro amesema uchaguzi katika mkoa wake ulienda vizuri isipokua changamoto mbalimbali zilijitokeza ikiwemo usafirishaji wa masanduku kutokana eneo la Delta.