.jpg?itok=YeAa_Mg_×tamp=1511516378)
Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo hii leo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Nyumba za walimu na ujenzi wa shule za Sekondari zilizopo kwenye wilaya ya Ilala ambapo tayari Wizara imetoa kiasi cha shilingi bilioni 5.6 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo.
Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako ametembelea na kukagua shule ya Sekondari Msongola, Nyumba za walimu, shule ya Sekondari Mvuti na shule kongwe ya Sekondari Pugu zote zilizopo katika manispaa ya Ilala, mkoani Dar es salaam.