Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa kuhusu jitihada za kimataifa wakati wa mizozo ya kiafya Jakaya Kikwete.
Akizungumza na idhaa ya Umoja wa Mataifa Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Tanzania amefafanua kuhusu mapendekezo ya jopo hilo kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa na akisisitiza kuhusu msaada wa kimfumo.
Kikwete amesema kuwa fedha nyingi zinatolewa na wahisani lakini hazitumi ipasavyo katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko bali zinaenda kutibu ugonjwa wenyewe kutokana na kushindwa kudhibiti dalili za magonjwa hayo.
Kikwete amesema kuwa kimfumo wa shirika la Afya duniani halina uwezo wa kukabiliana na mlipuko wa maradhi kutokana na kutopewa uwezo wa kwenda kubakibialana na maradhi kwenda kutoa misaada zaidi ya kutoa miongozo tu.
Aidha, amesema pendekezo la jopo hilo ni kuimarisha uwezo wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na hilo lilidhihirika zaidi wakati wa kushughulikia dharura ya homa kali ya Ebola Afrika Magharibi.