Wednesday , 16th Dec , 2015

Watu nane wamefariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Allys walilokuwa wakisafiria kupinduka katika kijiji cha vumilia Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suleiman Issa

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suleiman Issa amkesema ajali hiyo ilitokea jana alfajiri na kwamba basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Alfa Haji ambae alikimba baada ya tukio hilo.

Kamanda Issa amesema katika tukio hilo watu wanne kati ya nane ndio waliotambuliwa katika ajali hiyo ambapo katika watu hao waliofariki watano ni watu wazima na watatu ni watoto.

Kamanda Issa aliwataja Marehemu waliotambuliwa kuwa ni Grace Andrew,Pascal Abdul mwenye Umri wa miezi 8,Tipwege Kataga na Emiriana Tryphone wote wakazi wa Urambo.

Aidha Kamanda ameongeza kuwa Ajili hiyo ilitokana na mwendo kasi na utelezi katika barabara hiyo na kuwataka askari wa usalama barabarani kufuatilia madereva wazembe.