Ametoa kauli hiyo akiwa katika ziara yake mkoani Mtwara, akizindua Kituo cha Afya Mbonde kilichopo Masasi amesema,"watasema ninamjengea Mkapa, ndiyo namjengea Mkapa, kwa sababu bila Mkapa mimi nisingekuwa Waziri inawezekana pia Urais msingeniona, sasa kumjengea barabara tu hata siku akienda kuzikwa apite kwenye lami ni kosa?, najua Mkapa amenitoa wapi".
Kuhusiana na Waziri wa awamu ya tatu kupewa kiwanda cha korosho lakini hakiendelezi Rais Magufuli amesema, "kuna kiwanda naambiwa ni cha Waziri wa awamu ya tatu mumnyang'anye, akikataa shikeni pelekeni mahakamani hata kama alikuwa Waziri, tukibembelezana hatutafika ndugu zangu, tubembelezane mimi nikishamaliza muda wangu."
"Nitoe wito kwa waliouziwa viwanda vya kubangua Korosho na Serikali, ni lazima waanze kubangua Korosho na wazinunue, wakishindwa wavirudidhe viwanda, mfano yule wa Newala kiwanda hakifanyi kazi kabisa Waziri wa Kilimo mnyanganye hata kama ni leo.", amemalizia Rais Magufuli.




