
Akiongea na East Africa Television Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu ACP Boniventure Mshongi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akieleza kuwa ni ajali ndogo ya kawaida ambayo imesababishwa na vumbi kuzidi hali iliyopelekea gari moja kwenye msafara huo kugonga basi la abiria kwa nyuma.
''Ni kweli ajali hiyo imeripotiwa kwangu ila kwasasa nipo kwenye majukumu mengine na mkuu wa majeshi lakini taarifa nilizonazo ajali imetokea na ni ya kawaida, hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa vibaya, nitakapopata taarifa kamili nitawaeleza'', amesema Kamanda.
Aidha Kamanda Mshongi, ameeleza kuwa msafara huo ambao ulikuwa kwenye mwendokasi, ulizidiwa na vumbi kutokana na barabara za vumbi hivyo kusababisha gari hilo kugonga basi kwa nyuma lakini haikuleata madhara makubwa.
Zaidi msikilize Kamanda Mshongi akifafanua kwenye video hapo chini.