Hali ya taharuki imempata mwenyekiti mpya wa serikali ya mtaa wa Tabata na wajumbe wake kutoka chama tawala cha CCM baada ya kukabidhiwa ofisi ya mtaa huo ikiwa haina kitu chochote wala nyaraka zozote ambazo zimeachwa na mwenyekiti aliye pita kutoka chama hichohicho na hivyo kusababisha baadhi za kazi za kuwahudumia wananchi wa eneo hilo kusuasua.
Akizungumza na EATV mwenyekiti huyo na mjumbe wake wamesema kuwa walicho kabidhiwa na mtendaji ni muhuri mmoja tu ambao umevunjika ambapo wameiomba wizara husika kuyatolea matamko matatizo mengi yanayotokea baada ya uchaguzi kumalizika ambapo bila kufanya hivyo matatizo hayo yatajirudia katika vipindi vijavyo:
Nao baadhi ya wananchi ambao wamefika katika ofisi hiyo ili kupata huduma wameonesha jinsi walivyo kerwa na huduma za ofisi hizo ikiwemo kukaa kwa muda mrefu bila kuhudumiwa jambo ambalo wamesema limetokana na kutokuwepo kwa vifaa muhimu:.
Naye mwenyekiti wa serikali za mtaa aliyepita Hassan Chambuso akijibu tuhuma hizo amesema kuwa baada ya kumaliza kipindi chake ameondoka na nyaraka na samani kwa sababu vilikuwa vyakwake na hivyo kumtaka mwenyekiti huyo mpya ambaye naye ametoka chama cha mapinduzi CCM kama yeye anunue vitu vyake:.