Thursday , 28th Jan , 2016

Bunge la Afrika la Mashariki EALA,limeahirisha kujadili Muswada wa sheria ya kukabiliana na maafa na majanga wa mwaka 2013 hadi mwezi Machi mwaka huu baada ya kuzuka kwa mjadala mkali uliowagawa wabunge.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Mhe. Suzana Kolimba

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Mhe. Suzana Kolimba aliwasilisha ombi hilo ili ktoa mchango wa kisekta mbalimbali ambapo alitaka mswada huo ujadiliwe mwezi wa nane

Wabunge wengi walipinga hoja ya kuhairishwa kujadiliwa kwa muswada huo hadi mwezi wa nane kwa kusema kuwa muswada huo ni wa muda mrefu tangu ulipowasilishwa mwaka 2013.

Wakiongea kwa Nyakati tofauti mbunge wa bunge hilo kwa upande wa Tanzania, Shyrose Bhanji ameomba bunge hilo kumpa waziri huo muda wa kutosha kwani alikua mgeni katika wizara hiyo.

Kwa upande wake Judith Nayiai Pareno kutoka Kenya amesema baraza la mwaziri limechukua muda mrefu kuwasilisha mswada huo lakini wamesikitishwa na jinsi mawaziri hao wasivyoutendea haki muswada huo.