Tuesday , 16th Feb , 2016

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezindua basi la kwanza katika eneo la Afrika mashariki linalotumia nguvu za jua.

Basi hilo lenye viti 35 linatarajiwa kutumika mijini badala ya miji mikuu kutokana na masharti ya umbali wa usafiri wake.

Mabasi hayo yalitengezwa nchini Uganda na kampuni ya magari ya Kiira Motors Kayoola na
Yalionyesha kwa mara ya kwanza katika uwanja wa taifa Kampala mapema mwezi huu.

Mabasi hayo yalitengezwa nchini Uganda na kampuni ya magari ya Kiira Motors Kayoola na iwapo yatatengezwa kwa wingi, kila basi linaweza kugharimu dola 58,000.

Aidha moja ya betri zake inaweza kutiwa chaji ya miale ya jua vilivyopo katika paa la magari hayo ambavyo huongeza kasi ya gari hilo kufikia kilomita 80.

Chanzo BBC