Thursday , 15th Mar , 2018

Hosptali ya Taifa Muhimbili MNH imetakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika kupambana na rushwa kwa kusimamia haki ya mteja, kutimiza wajibu wa mtoa huduma, maadili ya taaluma na kutekeleza misingi ya utawala bora.

Hilo limesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hosptali hiyo, Dk Hellen Kondya wakati akizindua rasmi kamati ya uratibu na kamati ya kudhibiti uadilifu wa hospitali hiyo.

Dk. Kondya amesema ni muhimu kuweka, uhusiano kati ya majukumu ya kamati hizo na maadili ya kitaaluma ambayo yamebainishwa vyema katika sheria mbalimbali za taaluma za sekta ya afya.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema Hosptali hiyo imeunda kamati hizo ikiwa ni mwitikio wa utaratibu wa serikali unaozitaka idara za serikali na taasisi za umma kusimamia na kudhibiti uadilifu.