Thursday , 31st Mar , 2016

Halmashauri ya Mji wa Masasi Mkoani Mtwara imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kutoka vifo 22 vya mwaka 2014 mpaka kufikia vifo 12 mwaka 2015 ambapo ni sawa na asilimia 45 vya vifo vyote.

Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Halima Dendegu (kushoto) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkomaindo Dkt. Musa Rashid

Halmashauri ya Mji wa Masasi Mkoani Mtwara imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kutoka vifo 22 vya mwaka 2014 hadi kufikia vifo 12 mwaka 2015 ambapo ni sawa na asilimia 45 vya vifo vyote.

Akieleza mafanikio ya Manispaa ya Mji wa Masasi ,Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Masasi (Mkomaindo), Dkt. Mussa Rashid, amesema licha ya kupunguza vifo hivyo lakini pia wamefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kutoka asilimia 7.2 mwaka 2014 hadi asilimia 5 mwaka 2015.

Dkt. Rashid amesema kuwa idadi ya kina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya ni kubwa kutokana na uhamasishaji na elimu ya afya inayotolewa kwa akinamama na jamii juu ya umuhimu wa kujifungulia kwenye vituo vya Afya.

Dkt. Rashid alitoa takwimu hizo wakati akiwasilisha mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika sekta ya Afya katika Mji wa Masasi mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.