Monday , 27th Jun , 2016

Mkoa wa Mtwara umeanzisha mpango wa Benki ya Matofali ambao unatekelezwa katika ngazi za mitaa na vijiji, ili ifikapo mwezi Agosti mwaka huu walengwa watimize idadi ya matofali milioni moja katika kila mtaa na kijiji.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.

Akizungumza katika zoezi la kupokea madawati katika Shule ya Msingi Lilungu, Manispaa ya Mtwara Mikindani, kutoka kwa Shirika lisilo la kiserikali la Hassan Maajar Trust, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amesema lengo la mkoa ni kuona hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu ujenzi wa miundombinu hiyo unaanza.

Awali akisoma hotuba ya shirika hilo, Afisa Miradi, Bi. Kayemarie Bukila, amesema shirika hilo licha ya kukabidhi madawati 60 kwa shule mbili za Lilungu na Nanguruwe, limekabidhi vifaa vingine vya kujifunzia ikiwa ni pamoja na vitabu 181 na makabati manne, ambavyo jumla vina thamani ya sh. Milioni 1.2

Zoezi la utatuzi wa uhaba wa madawati linaendelea kutekelezwa katika halmashauri mbalimbali mkoani humo huku halmashauri ya mji wa Nanyamba ikiwa tayari imeshakamilisha kwa asilimia 100.