CAG Mussa Assad
Dk. Malecela ameweka wazi hayo zikiwa ni siku mbili kupita tangu Bunge la Tanzania kupitisha kutofanya kazi na CAG kutokana na kauli yake 'Bunge ni dhaifu' kwa madai ilikuwa na lengo la kulidhalilisha Bunge hilo.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Dk. Mwele ameandika kuwa yeye anasimama na CAG kwa kuwa ameweza kuonyesha bado kuna watu wakamilifu na yeye Assad akiwa ni mmoja wapo hasa katika kipindi hiki ambacho historia inaonyesha kwamba taifa lipo katika wingu jeusi.
Dkt Mwele ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, John Samuel Malecela amemwambia Prof Assad kwamba, "Historia itakukumbuka kama mtu wa heshima".




