Wednesday , 25th Jan , 2017

Mtoto, Lea Luchagula mwenye umri wa miaka 5 mkazi wa kitongoji cha Isengo kijiji cha Ilaji Kata ya Mahongole Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kuigonga Garimoshi ya abiria iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zambia.

Picha: Maktaba

Tukio hilo limetokea majira ya saa tano asubuhi wakati mtoto huyo akikatisha katika eneo la relini akitokea shuleni ndipo alipoigonga na kupoteza maisha papo hapo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Hamrid Moses Kahemele  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba ametoa taarifa kituo cha Polisi Igurusi ili waufanyie uchunguzi mwili wa marehemu ndipo wakabidhiwe ndugu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari alipotafutwa kuzungumzi tukio hilo hakupatikana kwani simu yake ya kinganjani iliita bila kupokelewa.