Mkuu wa wilaya ya Mtwara Wilmani Ndile amesema hayo baada ya wenyeviti wa mitaa, na wajumbe kula kiapo mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya Musa Esanju.
Amesema jamii yeyote ikifanya uongozi ni biashara, itambulike wazi viongozi hao hawatazungumzia matatizo ya watu bali watafanya yao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Rashindi Mtima amewataka wenyeviti hao kutambua kuwa jamii inawategemea hivyo hawana budi kulinda uaminifu huo kwa muda wa miaka mitano.
Kwa upande wao wenyeviti wa mitaa na wajumbe wakizungumzia nafasi hizo wamesema wataongoza kama ambavyo sheria inawataka na wataweka kando.