
Bobi Wine amesema kuwa lengo la uamuzi huo ni kumpinga Rais wa sasa wa nchi hiyo Yoweri Museveni, ambapo amedai atakuwa mgombea huru, kama ambavyo aliwania Ubunge akiwa hana chama cha siasa.
Aidha Bobi Wine, amedai kuna idadi kubwa ya viongozi katika Serikali ya Museveni wanamuunga mkono, wakiwemo Wabunge zaidi ya 60 wanaomshinikiza kuwania nafasi hiyo.
Bobi Wine alishawahi kukabiliwa na mashtaka ya uhaini, baada ya kukamatwa 2018, akituhumiwa kushambulia kwa mawe msafara wa Rais Museveni baada ya mkutano wake kumalizika.