
Philippe Corsaletti (kulia) akionesha maeneo ambako msafara huo utapitia, pembeni yake ni Bw. Raymond Tungaraza
Msafara huo unaanzia nchini Ugiriki na kuishia nchini Afrika Kusini na kupitia nchini
Mkuu wa Operesheni za Mafuta ya Ndege wa kampuni inayoratibu ujio wa msafara huo nchini ya Puma Energy Bw. Raymond Tungaraza, amesema hayo jijini Dar es Salaam leo na kwamba manufaa hayo yatatokana na msafara huo kukaa nchini kwa takribani siku tano huku marubani wakirusha ndege hizo katika maeneo ambako ndiko kwenye vivutio vya utalii.
Ujio wa msafara huo una baraka zote za Bodi ya Utalii nchini TTB ambapo kupitia kwa Msemaji wake Bw. Geofrey Tengeneza, amesema wanatarajia idadi ya watalii wanaokuja nchini itaongezeka kwani ujio wa msafara huo umevuta hisia kutoka maeneo mbalimbali duniani hasa kutokana na ukweli kwamba tukio hilo ni la aina yake kwani linahusisha ndege zenye umri wa zaidi ya miaka tisini.