Wednesday , 29th Apr , 2015

Waziri wa Ujenzi Dr John Magufuli amemtaka Mkandarasi anayejenga barabara ya mabasi ya kwenda kasi awamu ya kwanza toka Kimara hadi Kivukoni kampuni ya Strabag kumaliza sehemu ndigo ya kazi kwa haraka ili mradi huo uanze .

Waziri wa Ujenzi Dr John Pombe Magufuli.

Dr Magufuli ameyasema hayo katika ziara ya kukagua miundombinu ya mradi huo pamoja na kuweka jiwe la msingi wa barabara ya Uhuru awamu ya kwanza toka Msimbazi mpaka Makutano na barabara ya Kawawa,

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Meck sadick amemwomba waziri magufuli aendelea kuhudumia zaidi barabara za mkoa wa Dar es salaam ambao ni mji wenye watu wengi na shughuli nyingi za uchumi.

Naye mtendaji mkuu wa TANROADS mhandisi Patrick Mfugale yeye amewataka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo wa DARTS pamoja na barabara zote za jijini ili kuepusha gharama zaidi za kuhudumia barabara hizo zinazogharimu mabilioni ya fedha za Serikali.

Mradi wa DARTS wa awamu ya kwanza toka Kimara, Kivukoni, Magomeni, Moroco mpaka Kivukoni umekamilika na umegharimu Shilingi Bilion 322.015 huku Bilion 214.08 zikiwa zimelipwa tayari kwa mkandarasi.