Tuesday , 24th Jun , 2014

Baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeo nchini Tanzania wameibuka na kudai kwamba chama hicho kimekuwa kikikandamiza demokrasia ya kweli na hivyo kusababisha migogoro isiyo ya lazima.

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo - Chadema, Freeman Mbowe.

Madai hayo yametolewa jijini Dar es Salaam na viongozi hao Bw. Emmanuel Kitundu ambaye ni mwenyekiti wa baraza la vijana jimbo la wilaya ya Singida vijijini na Bw. Jacob Liviga ambaye naye ni mwenyekiti wilaya ya Lindi Vijijini katika mkutano wa waandishi wa habari.

Wakizungumza katika mkutano huo, viongozi hao wamesema bado ndani ya chama hicho hakujatokea mabadiliko na kwamba suala la demokrasia ambalo limekuwa likihubiriwa na chama hicho kwa muda mrefu bado ni changamoto.