Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsabahi rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Akizungumza kwa masikitiko mmoja wa watoto hao kwenye gesti hiyo, Liliani Peter (14), anayesoma darasa la nane, amesema wao walirudi shuleni Mei 4 mwaka huu na Mei 16 walirudishwa nchini baada ya kuelezwa na mwalimu mkuu wa shule yao Abel Githinji kuwa hawatakiwi kuwepo Kenya mpaka maelewano yatakapopatikana baina ya Tanzania na Kenya.
Liliani amesema kuwa wao baada ya kumuuliza mwalimu mkuu wao sababu ya kuwafukuza Kenya, walijibiwa kuwa watanzania wamewapiga raia wa Kenya hivyo nanyi hamtakiwi huku rudini Tanzania mpaka mapatano yatakapopatikana.
Naye Elikana Tayai (8) wa darasa la kwanza, amesema alisikia wakisema wenzao watanzania hawatakiwi Kenya na tunatakiwa kurudi kwetu na tukapakizwa katika magari kuridi huku.
John Laize (13) darasa la nane shule ya Naikara nchini Kenya, amesema wamerudishwa na wenzao wanaendelea na masomo kama kawaida, hivyo wanaomba Tanzania wamalize mgogoro huo ili waweze kurudi masomoni.
Amesema wao waliofanikiwa kurudi nchini ni wale wanaofadhiliwa na Seminari, kwa wenzao ambao wanasomeshwa na wazazi wao, wamebaki katika shida na hatma yao haijulikani.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo ni zoezi la kamata-kamata ya wahamiaji haramu toka nchini Kenya lililofanyika Mei 12 mwaka huu.
Alisema serikali ilipata taarifa za kuwepo wahamiaji haramu na waliendesha zoezi na kufanikiwa kuwakamata watu 17 toka Kenya, ambao wawili kati yao walikuwa watoto wadogo na walikabidhiwa kwawazi wao na mmoja mfanyabiashara aliachiwa baada ya mahojiano na watu wazima walifikishwa mahakamani.
Amesema baada ya zoezi hilo kufanyika Mei 12 walikaa kikao serikali ya Tanzania na viongozi wa Kenya na Tanzania kwa lengo la kutengeneza ujirani mwema na kukubaliana mambo ya msingi matatu.
Mgandiliwa amesema walikubaliana Kenya waruhusu wafanyabiashara kuja nchini na sisi kwenda kwao kufanya biashara kwa kuwaandikia kibali cha siku saba cha kuishi Tanzania au Kenya, kitu cha pili tulikubaliana tuwaruhusu wafugaji waje wakati wa ukame kulisha mifugo kwa kibali hicho na wanafunzi waliofukuzwa warudishwe Kenya na wakafikia muafaka.
Mgandilwa amesema ghafla akasikia wanafunzi wetu wamerudishwa wakiambiwa mpaka wakae viongozi wa kimila wa huku Tanzania na Kenya Mei 23 mwaka huu wazungumze ndipo wanafunzi warudi shuleni na sasa anamtafuta mkuu wa wilaya ya South Naroki nchini Kenya wazungumzie suala hilo.