Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein, akiwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kisiwani Zanzibar, alipomtembelea mmoa wa majweruhi wa tukio la kumwagiwa tindikali.
Akiongea jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Bodi ya wakala katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali Prof: David Ngasapa amesema wamejipanga kupambana na uingizwaji wa kemikali kinyume na taratibu kwa kuweka mitambo maeneo ya mipakani ya kubaini uingizwaji wa kemikali hizo zoezi litakaloenda sambamba na kuwekwa kwa vituo maalum vya ofisi ya mkemia mkuu wa serikali.
Kwa upande wake mkemia mkuu wa serikali Prof: Samweli Manyele amesema wanachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha wafanyabiashara wa kemikali wanapewa elimu ya kuelewa kwamba ni lazima kemikali zote zinazoingia hapa nchini ofisi ya mkemia mkuu wa serikali itambue na kutoa kibali cha kemikali hizo.