Friday , 8th Jan , 2016

Ukosefu wa mitaji na elimu za Kibiashara unasababisha wafanyabishara mkoani Kigoma ,kushindwa kutumia fursa za kibiashara zilizopo kutokana na kupakana na nchi za Congo DRC, na Burundi ambazo zinategemea mahitaji mengi ya bidhaa kutoka nchini.

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo mkoani Kigoma (TCCIA). Ramadha Kabuga

Hayo yameelezwa na makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo mkoani Kigoma (TCCIA). Ramadha Kabuga wakati akieleza mpango wa taasisi hiyo kutoa mkopo wa shilingi bilioni moja kwa chama cha kuweka na kukopa cha muungano cha mjini Kigoma.

Bw. Kabuga amesema uwepo wa bandari ,reli ya kati na barabara zilizoanza kujengwa kwa kiwango cha lami kunapaswa kwenda sambamba na kukuza uwezo wa wajasiriamali kumudu soko na mahitaji ya kibiashara ya nchi jirani

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano Saccos Sadi Ibrahim amesema zaidi ya wanachama mia tatu wa saccos hiyo ambao wengi ni wafanyabiashara na wajasiriamali wanatarajiwa kunufaika na mkopo wa shilingi bilioni 1.5 kutoka TCCIA na benki ya CRDB, mikopo itakayowasaidia kuboresha bidhaa na kuwa na uwezo wa kusafirisha kutafuta soko ndani na nje ya nchi.