Monday , 22nd Feb , 2016

Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga inakabiliwa na changamoto ya Mimba za utotoni kuanzia umri wa miaka 14 hadi 17 na kushindwa kuendelea na masomo kutokana na ndoa za utoto na kutokujua elimu ya Afya ya Uzazi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Husna Rajab Msangi

Akiongea wilayani humo Meneja na mratibu wa mradi wa Afya kwa kijana wa leo uliozinduliwa na viongozi wa serikali kwa ajili ya kudhibiti tatizo hilo Dkt. Aisha Byanako amesema lengo la mradi huo ni kupunguza kazi ya mimba za utotoni.

Dkt. Aisha ameongeza kuwa mradi huo utalenga zaidi kutoa elimu kwa vijana kuanzia wenye umri wa miaka 10 hadi 24 ili kudhibiti afya ya vijana hao ambao ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Husna Msangi amewataka wakazi wa Kata ya Kang'ata kuacha kujiingiza katika vitendo vya ndoa za utotoni ambapo takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi moja wapo iliyoathirika zaidi na tatizo hilo.