Friday , 22nd Jan , 2016

Jeshi la polisi mkoani Njombe limekusanya zaidi ya shilingi milioni 17 ikiwa ni tozo la faini kwa madereva wa pikipiki na magari wanao kiuka taratibu za usalama barabarani katika oparesheni yao ya siku chache iliyoanza mwanzoni mwa mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Wilbrod Mtafungwa

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe John Temu alisema kuwa Jumla ya pikipiki 445 na magari 150 yalikamatwa na kukutwa na makosa na kutozwa tozo.

Hata hivyo amesema kuwa katika oparasheni hiyo kulikuwa kukiangaliwa watu wanao endesha bila leseni, kupakiza abiria zaidi ya mmoja, kutovaa Helmeti kwa pikipiki, kuchanganya abiria na mizigo, mwendo kasi, pamoja na kupakia mizigo hatari.

Ameongeza kuwa madereva wa bodaboda wamekuwa wakipewa elimu mara kadha lakini wamekuwa hawaelewi, na kuongeza kuwa madereva hao wahakikishe kuwa wanafuata sheria za barabarani.