
Naibu Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha
Ole Nasha ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro ameyasema hayo aliposhiriki hafla ya jamii ya kimasai mkoani Arusha ya kuwaaga vijana ambao wamemaliza muda wa kutumika kama jeshi la kabila la wamaasai na kuwa watu wazima,.
“Mila zetu zinaweza kuleta maadili mazuri katika jamii, tuendelee kulinda na kutetea mila zetu hasa zile zenye kuleta maendeleo katika jamii yetu” Amesema Ole Nasha
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji wilayani Ngorongoro, Edward Maura, amewataka vijana ambao wamemaliza hatua ya ujana na kukaribishwa kuwa watu wazima kuendelea kuisaidia jamii katika kutunza mila na desturi za kimaasai.