Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa SSRA, Bw. Honorius Nkole amesema, kwa kuanzia watafungua mfuko maalum kwa ajili ya madereva wa daladala na bodaboda kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma za mifuko ya jamii.
Aidha makundi mengine yatakayonufaika na mfuko huo ni pamoja na mama lishe na madereva daladala ambapo wataweza kunufaika na mafao ya uzeeni, matibabu pamoja na mikopo itajkayowawezesha kukuza mitaji yao.