Monday , 1st Aug , 2016

Umoja wa watengenezaji mifuko iliyo rafiki wa mazingira jijini Dar es salaam (UWAMITA) leo umezindua kampeni yake ya kugawa mifuko hiyo bure kwa wafanyabiashara katika masoko mbali mbali ya manispaa ya Ilala

Umoja wa watengenezaji mifuko iliyo rafiki wa mazingira jijini Dar es salaam (UWAMITA) leo umezindua kampeni yake ya kugawa mifuko hiyo bure kwa wafanyabiashara katika masoko mbali mbali ya manispaa ya Ilala ili kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imekuwa ikichangia uchafuzi wa mazingira.

Mwenyekiti wa umoja huo Bw. Jumanne Maulidi amesema kampeni hiyo inalenga pia kutekeleza agizo la serikali la kuzuia mifuko hiyo kutumika kwa kuwekea vyakula hasa vile vya moto ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kumpata binadamu kutokana na kemikali zinazotumika kutengeza mifuko hiyo.

Nao baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki kupokea mifuko hiyo wamesema wanaunga mkono hatua ya taasisi hiyo ya kugawa mifuko hiyo jambo ambalo wamesema itasaidia kupunguza tatizo la uchafu unaotokana na mifuko hiyo.