Saturday , 25th Jun , 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemteua Mhandisi Deusdedit Conatus Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA).

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu wa Wazir , Bw. Ramsey Kanyanga imesema kuwa uteuzui huo umeanza mapema tarehe 25 Juni.

Mhandisi Kakoko amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw Ephraim Mgawe ambae uteuzi wake ulitenguliwa, na kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kakoko alikuwa Meneja wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).