Monday , 22nd Sep , 2014

Walimu wa shule za msingi na sekondari Jijini Tanga nchini Tanzania wametangaza Kufanya mgomo endapo mapendekezo yao kwa wizara ya Kazi na Ajira hayatashughulikiwa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Dkt Shukuru Kawambwa.

Mapendekezo hayo ni pamoja na kuitaka Mamalaka ya Hifadhi ya Mifuko ya Jamii nchini - SSRA, kuachana na kupunguza mafao kwa wafanyakazi wastaafu wakiwemo walimu.

Akizungumza katika kikao maalumu cha kujadili pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CWT jijini Tanga Damiani Mabena amesema mapango wa serikali wa kupunguza mafao ya wastaafu wakiwemo walimu wamesema utachangia kushusha kiwango cha elimu na kuiomba serikali isifikirie kupitisha sheria hiyo kwa kuwa itakuana athari kwa jamii nzima.

Kwa upande wa viongozi wa CWT Taifa walioshirikia mkutano wametoa tamko kwa vyama vya walimu katika mikoa mingine kuunga mkono kupinga azma hiyo kwa nchi nzima na kusema mpango huo wa serikali ni wenye dhuluma na unadhoofisha maendeleo ya Elimu.