Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kilolo Bw. Brayan Kikoti
Bw. Kikoti amesema ikiwa wananchi wa Kilolo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao atahakikisha wazee wanapata bima za afya.
Bw. Kikoti amewakumbusha wananchi kuchagua kiongozi ambaye atasimamia rasirimali zilizopo katika jimbo hilo ili ziwanufaishe watu wote bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.
Naye Mgombea nafasi ya udiwani kata ya Dabaga Bw. Octavian Lukosi ameahidi kuitisha mikutano ya mara kwa mara kusikiliza kero za wananchi ikiwa atachaguliwa.
Hata hivyo, wagombea hao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameahidi kusimamia rasilimali za jimbo la Kilolo ili kuwanufaisha wananchi wote.