Monday , 8th Feb , 2016

Mfumuko wa bei chashuka kutoka asilimia 6.8 mwezi Desemba mwaka jana hadi asilimia 6.5 mwezi Januari mwaka huu.

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Tanzania kimeshuka kiasi kutoka asilimia sita nukta nane ilivyokuwa mwezi Disemba mwaka jana hadi asilimia sita nukta tano mwezi Januari mwaka huu.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo, amesema hayo jijini Dar es salaam leo na kwamba takwimu hizo zimetokana na marekebisho ya mwaka wa kizio cha ukokotoaji kutoka mwaka 2010 hadi 2015.

Kwa mujibu wa Bw. Kwesigabo, hata thamani ya shilingi nayo imebadilika ambapo shilingi mia moja hivi sasa inaweza kufanya manunuzi yenye thamani ya shilingi 99.3.