Tuesday , 10th Mar , 2015

Mfumuko wa Bei za bidhaa na huduma kwa mwezi februari mwaka2015 umeongezeka hadi 4.2% toka 4.0% ukilinganisha na mwezi januari2015.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini.

Kupanda kwa mfumuko wa bei kunachangiwa na kupanda kwa kasi ya bei za huduma na bidhaa ukilinganisha na kasi ya bei hizo mwaka februari2014.

Akiongea na waandish wa Habari ofisini kwake Mkurugenz wa Sensa na Takwimu za kijaa Ephraimu Kwesigabo toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS ameongeza kuwa bidhaa zilizopanda sana ni pamoja na Mchele kwa 18.5%, samaki kwa 12.4% na maharagwe kwa asilimia 7.1%, huduma ya kumwona daktari 11.2%, bei hizi zilipanda ukilinganisha na mwezi februari mwaka2014,

Kwa Upande wa Uwezo wa Shiling mia wa kununua bidhaa umeshuka na kufika sh. 64 na senti59 mwezi februari2015 kutoka septemba 2010 ambapo ilikuwa sh. 65 na senti60