Monday , 9th Feb , 2015

Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania NBS imesema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Januari mwaka huu umeshuka na kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ya mwezi wa Desemba mwaka jana.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania NBS imesema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Januari mwaka huu umeshuka na kufikia asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.8 ya mwezi wa Desemba mwaka jana.

Akizungumzia kushuka kwa mfumuko wa bei leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za jamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo amesema kushuka huko kunatokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi Januari.

Kwesigabo amesema bidhaa hizo ni pamoja na kushuka kwa bei ya mahindi,unga wa mahindi, samaki na Mihogo pamoja na kushuka kwa bei ya nishati ya mafuta ikiwa ni pamoja na Mafuta ya taa.

Kwa upande mwingine, Pamoja na thamani za Hisa za makampuni makubwa kupanda katika Soko la hisa la Dar es salaam DSE, Bado mauzo sokoni hapo yameshuka kwa kwa asilimia 55.57 kutoka shilingi za Tanzania Billion 84 hadi kufikia shilingi bilioni 37..

Akizungumza na waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa Soko hilo la hisa la Dar es salaam DSE Afisa Maendeleo ya kibiashara Aleck Ngoshani amesema sekta ya Viwanda imeongoza kwa kuchangia asilimia 94.5 ya mauzo yote sokoni huku sekta ya kibenki ikichangia kwa asilimia 5.28,ambapo benki ya CRDB ikichangia asilimia 3.50 pekee huku sekta ya Biashara na Huduma ikichangia kwa asilimia 0.00.

Makampuni ambazo thamani za hisa zao zilipanda ni Pamoja na TBL, CRDB