Monday , 8th Jun , 2015

Wizara ya ardhi nchini Tanzania imesema imeanza mkakati ujenzi wa mfumo wa kielekroniki wenye lengo la kuhifadhi kumbukumbu za ardhi na kukadiria kodi ya ardhi.

Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2015/16 ya wizara ya ardhi nyumba na maendeleo na makazi Mh William Lukuvi amesema mfumo huo una lengo la kuhifadhi kumbukumbu za ardhi pamoja na kupokea taarifa na kuwafikia wananchi kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi ambapo watatumia simu katika kutoa taarifa za masuala ya migoro ya ardhi.

Amesema kupitia mfumo huo umesaidia katika kufahamu kero za ardhi pamoja na kuwatuma wataalamu na kuwa wataendelea kupambana na watendaji wasio waaminifu na wasio na maadili na wanaosababisha kero kwa wananchi na kuwatahadharisha matapeli wa ardhi wakiwemo wale wanaojiita madalali.

Hata hivyo Lukuvi amesema wizara imeandaa mkatati wa ulipaji fidia kwa wadai na kuongeza kuwa kuanzia wiki ijayo atakutana na wananchi waliopo katika maeneo yenye mgogoro jijini Dar es salaam ya Chasimba na Makongo Juu ili kuweza kupata muafaka wa kudumu katika maeneo hayo.