
Meya wa Manispaa Iringa mjini Alex Kimbe.
Alex Kimbe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jaffo kuomba radhi kwa Chama Cha Madaktari kumwajibisha daktari kinyume na sheria.
“Kwa kiongozi mzuri anapaswa ajitafakari, kama Waziri ameomba radhi kwa niaba yake yeye pia Mkuu wa Mkoa aombe radhi, lakini pia unakumbuka mambo yaleyale ambayo sisi tuliyasema kwamba anakiuka sheria”, amesema Kimbe.
Aidha Kimbe amesema “hili tukio ni mara ya pili linafanyika iringa, kwa mujibu wa sheria anayewajibisha ni halmashauri na wizara, lakini sio Mkuu wa Mkoa kuhalalisha moja kwa moja kwamba mtumishi yule alikosea, na ndo maana mpaka sasa unaona Waziri ameomba radhi.”
Hivi karibuni Waziri Selemani Jafo alikiomba radhi Chama cha Madaktari (MAT) kwa niaba ya RC Iringa, Ally Hapi na kuahidi kuwaandikia barua viongozi wa kisiasa kufuata sheria kuwawajibisha watumishi.