Friday , 18th Apr , 2014

Meli ya mizigo ya Kampuni ya FB Matara iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza ikiwa na wafanyakazi kumi na shehena ya sukari imezama ziwa victoria katikati ya visiwa vya Kerebe na Bumbile.

Sehemu ya Ziwa Viktoria

Meli ya mizigo ya Kampuni ya FB Matara iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza ikiwa na wafanyakazi kumi na shehena ya sukari imezama ziwa victoria katikati ya visiwa vya Kerebe na Bumbile.

Meli hiyo ilikuwa ikitoka katika kiwanda cha sukari cha Kagera ikiwa na tani 280 za sukari ambazo zote zimezama katika eneo hilo lililoko Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Watu wote waliokuwemo wameokolewa na shughuli za kuiopoa meli hiyo zinaendelea.