Wednesday , 9th Jul , 2014

Mbunge wa viti maaluma Arusha Catherine Magege ameiomba serikali kuanzisha kanda maalumu ya kipolisi kwa jiji la Arusha ili kuimarisha ulinzi ambao umekuwa ukizorota siku hadi siku huku maisha wa wakazi wake yakiwa hatarini.

Mkuu wa polisi nchini IGP Ernest Mangu.

Kufuatia mfululizo wa mabomu baadhi wa kazi wa jiji la Arusha wameiomba serikali kuingilia kati swala hilokwa kuwa watu wamekuwa na hofu ya kushiriki katika matukio mbalimbali hasa yale ya mikusanyiko ya watu kwa kuhofia milipuko.

Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashikilia watu wawili kuhusiana na mlipuko uliotokea katika Mgahawa wa Vama Traditional Indian Culture uliopo karibu na viwanja vya Gymkhana na Mahakama Kuu Jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Makosa ya jinai nchini Tanzania DCI Issaya Mngulu ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar-es-Salaam huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari wawapo kwenye mikusanyiko.